Rais wa Marekani, Joe Biden amelihutubia taifa la nchi hiyo na kuzungumzia juu ya tishio kwa demokrasia ya Amerika, akionya kwamba maadili ya nchi hiyo yanashambuliwa na watiifu wa Rais wa zamani Donald Trump.

Akiongea kupitia luninga, Biden amesema, “Kwa muda mrefu, tumejihakikishia kuwa demokrasia ya Amerika imehakikishwa lakini sivyo na sasa tunapaswa kuitetea, kuilinda na kuisimamia na hili ni jukumu la kila mmoja wetu.”

Kwa maelezo ya moja kwa moja, Biden aliufafanua uchaguzi ujao wa katikati ya muhula kama vita kwa nafsi ya taifa na kuwashutumu Warepublican watiifu kwa Trump kwa kukumbatia misimamo mikali na kudhoofisha maadili ya kidemokrasia.

Rais wa Marekani, Joe Biden wakati alipokuwa akilihutubia Taifa. Picha na Doug Mills/The New York Times.

Ametoa mfano kwamba, “majaribio ya ajabu ya kujitawala” yaliyowakilishwa na Katiba, Biden alisema kwamba “historia inatuambia uaminifu wa kipofu kwa kiongozi mmoja na nia ya kushiriki katika vurugu za kisiasa ni mbaya kwa demokrasia.”

Kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula, Biden amechukua muda mchache kutaka maelewano na muda mwingi kuwashutumu Republican kwa kuwasilisha hatari kwa demokrasia, akitumia baadhi ya lugha kali na za kivita katika matamshi yake.

Prince Dube aisubiri kwa hamu Young Africans
Ukame, Njaa yasambaratisha Familia Mil. 1