Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Kenya Harrison Mwendwa ameachana na Klabu ya Singida Big Stars, baada ya kusajiliwa mwezi mmoja uliopita.

Kiungo huyo aliyehusishwa na klabu za Simba SC, Young Africans na Azam FC alitua nchini akitokea kwao Kenya mwezi Julai, alisajiliwa Singida Big Stars kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kocha Msaidizi wa klabu hiyo inayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara Mathias Lule amesema kiungo huyo amelazimika kuachwa, kufuatia mapendekezo ya Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha kutoka Uholanzi Hans van der Pluijm.

Amesema Mwendwa alifanyiwa majaribio mara kadhaa kabla ya kuingizwa kwenye kiksoi cha kwanza cha Singida Big Stars, lakini kiwango chake cha soka hakiendani na mfumo wa Kocha Hans.

“Ni kweli tulimpa mkataba ila baada ya kutoridhishwa na kiwango chake tumeamua kuachana naye, tuligundua timu aliyotoka alikaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha na alipofika hapa alishindwa kuendana na kasi ya wenzake.” amesema Lule

Kabla ya kutua nchini Mwendwa alikua akiitumikia klabu ya Kabwe Warriors inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia.

Milton Karisa aichimba mkwara Taifa Stars
PICHA: Simba Queens yakabidhiwa basi jipya