Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar (ZFF), leo Ijumaa (Septemba 02) limeingia Mkataba wa Ushirikiano wa miaka mitano na Kampuni ya Jackson Group Sports.

Mkataba huo unahusisha huduma za masoko zitakazowavutia wawekezaji wakubwa kwa ajili ya kuwekeza katika soka la visiwa hivyo.

Sehemu ya makubaliano ya mkataba uliosainowa, Kampuni Jackson Group Sports itakuwa na asilimia 15, huku ZFF ikipata asilimia 85.

Huu ni mkataba wa pili kwa Kampuni ya Jackson Group Sports kuusaini mwaka huu katika mchezo wa Soka, wakitangulia kufanya hivyo na klabu ya Young Africans mwezi Agosti jijini Dar es salaam.

Young Africans iliingia mkataba wa ubia wa kimasoko (Marketing Partnership) na Kampuni ya Jackson Group kwa kipindi cha miaka miwili.

Jackson Group ni kampuni ya kitanzania inayojihusisha na uwakala wa masoko nchini Tanzania na huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi wa haki za IP (IP rights management) pamoja na kufanya kazi na wadau wanaojihusisha na udhamini kwenye michezo wakiwa na uzoefu mkubwa wa kufanya kazi na wadhamini wa ndani, Afrika na Ulaya.

Mabadiliko sheria ya Habari yatoa 'mwanga wa matumaini'
Kenya: Wakili atoa ushahidi wa Mvenezuela kushiriki uchaguzi