Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amewataka baadhi ya watu kuacha kupotosha taarifa zinazotolewa na Serikali juu ya wapimaji wa ardhi ambao wamekuwa wakitumia madhaifu ya Ofisi za ardhi kujinufaisha na kuwakandamiza Watanzania.

Waziri Mabula, ameyasema hayo katika siku ya pili ya mkutano wa Wadau wa Sekta ya milki Tanzania, ulioanza jana Septemba mosi, 2022 na unaofikia tamati hii leo Septemba 2, 2022 jijini Dar es Salaam.

Amesema, katika tamko lake hapo jana alisema Serikali inatarajia kuchukua hatua dhidi ya kampuni zinazoleta migogoro kwa wananchi kwa kuwapimia watu vipande vidogo vidogo vya ardhi isiyopimwa, bila kujali suala la mipango miji na athari zinazoweza kujitokeza hapo baadaye.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula.

Mabula amefafanua kuwa, baadhi ya wapimaji wa ardhi wamekuwa wakishiriki kuwauzia wananchi vipande vidogo kwa bei kubwa na kisha kuwaelekeza wanunuzi hao kwenda ofisi za ardhi ili kupimiwa viwanja hivyo hali wakijua kufanya hivyo ni makosa kisheria.

Nimefuatilia mijadala inayoendelea na kupitia mkutano huu na bahati nzuri vyombo vya habari vipo hapa, niwaombe waache kupotosha taarifa, kuna watu wanapima viwanja vidogovidogo na wanauza milioni saba au zaidi, msitumie madhaifu ya ofisi za Serikali kujinufaisha,” amefafanua Waziri Mabula.

Akifungua mkutano huo hapo jana, Waziri Mabula alisema, “Mpimaji yeyote atakayepitisha viwanja vya mita 300 au 500 atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kuanzia leo Sept. Mosi 2022 kwani hatua hiyo inawafanya wananchi kushindwa kufanya mipango yao kwa kukosa eneo stahiki linalotambulika kiukubwa kwa mijibu wa taratibu,” amefafanua Dkt. Mabula.

Washiriki katika moja ya mikutano na Waziri wa Ardhi.

Aidha aliongeza kuwa, kitaaluma hakuna viwanja vya nna hiyo na wala havikubaliki na vinaaibisha taaluma ya mipango miji kutokana na tamaa ya baadhi ya watu ambao hujichukulia maamuzi bila kujali athari zinazoweza kujitokeza.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mabula akazielekeza bodi ya usajili mipango miji na ile ya usajili wa uthamini kufanya tathmini na kuchukua hatua na makampuni ya upimaji au mtu anayepima vipande vya ardhi waache haraka na warudishe fedha za wananchi na kuwataka wananchi kupata taarifa au maelekezo na ushauri kwa ofisi za ardi kabla hawajanunua ardhi husika.

Rais aridhia Mkurugenzi Mkuu ZAECA kujiuzulu
Mabadiliko sheria ya Habari yatoa 'mwanga wa matumaini'