Mahakama ya Juu ya Kenya imesikiliza hoja za kupinga uchaguzi wa urais ambayo iliwasilishwa na mgombea wa upinzani na kiongozi wa azimio la umoja kwanza, Raila Odinga kutokana na madai ya uwepo wa matatizo mbalimbali ya mchakato wa uchaguzi.

Katika uchaguzi huo, Tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC, chini ya Mwenyekiti wake Wafula Chebukati ilimtangaza Naibu Rais wa Kenya William Ruto kuwa mshindi kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Mahakama inapaswa kutoa uamuzi kuhusu changamoto zote kufikia Jumatatu Septemba 3, 2022 ambapo Odinga anadai kuwa mchakato huo ulikumbwa na uhalifu na anataka matokeo yafutwe na kuitisha uchaguzi mpya.

Uchaguzi huo wa amani uligeuka kuwa wa machafuko katika dakika za mwisho kabla ya tamko hilo wakati tume ya uchaguzi ilipogawanyika na makamishna wengi walisema hawawezi kuunga mkono matokeo.

Jaji, Martha Koome.

Makamishna hao wanne, waliopingana na mwenyekiti walilalamikia juu ya utovu wa nidhamu, na kuendeleza kutokuwa na uhakika wa demokrasia thabiti zaidi katika Taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kufikia wakati huo, uchaguzi huo ulikuwa ukionekana kuwa wa uwazi zaidi, huku tume ikichapisha fomu za matokeo zaidi ya 46,000 mtandaoni kutoka vituo vya kupigia kura ili mtu yeyote afanye hesabu mwenyewe.

Lalamiko jingine ni juu ya dhamira ya IEBC ya kupotosha utashi wa uhuru wa watu wa Kenya na kupindua utaratibu wa kikatiba kwa kutangaza matokeo ambayo hayakuwa yamehesabiwa na kuthibitishwa kikamilifu.

Mwanasiasa, Raila Odinga.

Inaarifiwa kuwa, maeneo ya ubunge 27 yanayodaiwa kuachwa na kura zake kutohesabiwa, yangeleta badiliko katika matokeo, ombi ambalo linapendekeza kuangalia kipengele hicho kama moja ya mapungufu.

Madai ya udukuzi wa baadhi ya fomu za matokeo na data za kompyuta pia yamejadiliwa, na inasemekana hatua hizo zilileta mabadiliko katika uchaguzi wa karibu ambapo Odinga alipata karibu 49% ya kura.

Watoto Mil. 244 wakosa haki ya masomo
Waliotengana na familia 'wafunguka' mazito