Takwimu mpya za UNESCO zinaonyesha kuwa watoto na vijana milioni 244 kati ya umri wa miaka 6 na 18 Duniani kote, bado hawako shuleni na kupelekea shirika hilo kutoa wito wa uhamasishaji wa pamoja ili kuhakikisha kuwa haki ya kila mtoto kupata elimu bora inaheshimiwa.
Taarifa hiyo inasema, kati ya watoto milioni 244 wenye umri wa miaka 6 hadi 18, wasio shuleni ni zaidi ya asilimia 40 na milioni 98 kati yao wanaishi Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo nchini Nigeria (milioni 20.2), Ethiopia (10.5), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (5.9) na Kenya (1.8).
UNESCO inadai kuwa, wasichana wengi wameacha shule kuliko wavulana mwaka 2000 (zaidi ya asilimia 2.5 kwa shule ya msingi, zaidi ya asilimia 3.9 kwa shule ya upili), huku pengo la kijinsia likikiwa ni sifuri.
Zaidi ya watoto milioni 400 hawakuenda shule mwaka 2000, kulingana na taasisi ya kimataifa, ambayo inakaribisha “maendeleo” katika eneo hili katika miongo miwili iliyopita, hata kama kasi “imepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.
Hata hivyo, kwa msaada wa UNESCO, asilimia 90 ya nchi zimeweka vigezo vya kitaifa vya kutathmini maendeleo kuelekea elimu bora kwa wote ifikapo 2030, ikiwa ni pamoja na viwango vya nje ya shule.