Kocha Mkuu wa Muda wa Simba SC Juma Mgunda amewataka Wachezaji wake kuelekeza akili zao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons na kuachana na Nyasa Big Bullet ya Malawi.

Simba SC itakua Mgeni wa Tanzania Prisons kesho Jumatano (Septemba 14), kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya kuanzia saa kumi jioni.

Mgunda aliyekabidhiwa kijiti cha kuliongoza Benchi la Ufundi la Simba SC akichukua nafasi ya Kocha Zoran Maki aliyekubali kuvunja mkataba wake juma lililopita, amesema kuna haja kwa wachezaji wake kufikiria na kusadiki kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Prisons na kuachana na Nyasa Big Bullet ambayo watakipa nayo Jumapili (Septemba 18).

“Mchezo wa Mkondo wa Kwanza dhidi ya Nyasa Big Bullet umekwisha, tutacheza nao tena Jumapili hapa Dar es salaam, kilichopo mbele yetu ni Mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons, wachezaji wangu wanapaswa kuelekeza akili zao kwenye mchezo huu,”

“Kuufikiria mchezo wa Mkondo wa Pili dhidi ya Nyasa Big Bullet ambao utakua mwishoni mwa juma litakua kosa kubwa, akili zinapaswa kuwa Mbeya kwenye mchezo wa Ligi Kuu kwanza, tukimaliza tutaanza kufikiria namna ya kumaliza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.”

“Tunafikiria ya Mbeya kwanza, ni muhimu sana kwetu kushinda, Simba SC kiu yake ni mafanikio ya kupata alama tatu za mchezo huo, nimezungumza vizuri na wachezaji wangu naamini wamenielewa na watafanya kazi ya kupambana ili kutuletea ushindi.” amesema Mgunda

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana msimu uliopita katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Simba SC ilikubali kupoteza kwa 1-0, bao likifungwa na Benjamin Asukile.

Jukumu la kwanza la Rais mpya wa Kenya EAC
Benjamin Asukile aitahadharisha Simba SC