Jumla ya Watoto wa kike 40 wameandaliwa mafunzo ya kuongeza uwezo wa kujiamini, kutambua afya ya akili, kukuza ustawi katika masuala ya lishe na ukakamavu, haki za mtoto wa kike na ufahamu wa sheria zake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Mkurugenzi wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete, Vanessa Anyoti imesema mafunzo hayo yamepewa jina la “Wasichana Washika Hatamu” yakiwa ni jukwaa la kuwapa mafunzo Watoto wa kike kuongeza uwezo huo wa kujiamini, kutambua afya ya akili, kukuza ustawi wao.
Amesema, “Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike imekuwa jukwaa muhimu katika kutambua haki za msichana pamoja na changamoto kubwa anazopambana nazo duniani, na kwamba sasa kuna wito wa kuchukua hatua za kuleta mageuzi ya kijamii na kisiasa, ili kuondoa vizuizi mbalimbali vya ubaguzi na chuki vinavyoendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wasichana.”
Mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi za Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF), ikishirikiana na Plan International Tanzania, kama sehemu ya shughuli za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani, yanayotarajia kutafanyika Septemba 24, 2022 katika jijini Dar es salaam cvhini ya kauli mbiu isemayo, “Wakati wetu ni sasa – haki zetu, mustakabali wetu.”