Mlinda Lango wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Djigui Diara amewatoa hofu Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kuhusu maendeleo ya afya yake.
Diara alipata Majereha wakati wa mchezo wa Mzunguumo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania, uliopigwa jijini Arusha na Young Africans ilishinda 2-1.
Hata hivyo Mlinda Lango huyo alikosa mchezo dhidi ya Coastal Union, na kurejea tena dimbani dhidi ya Azam FC lakini hali ilimuendea kombo katika mchezo wa mwisho dhidi ya Zalan FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akiwa katika kambi ya timu ya taifa ya Mali, Diara amesema anaendelea vizuri na tangu alipojiunga na wenzake mwanzoni mwa juma hili, amekua akifanya mazoezi baada ya kufanyiwa vipimo na jopo la Madtari.
“Kwa sasa ninaendelea vizuri baada ya huduma za kitabibu ambazo nimepewa tangu nikiwa na timu ya madaktari wa Young Africans, lakini pia hata nilipojiunga na kikosi cha timu ya taifa nilifanyiwa vipimo na waliridhishwa na maendeleo yangu.”
“Tayari nimenza mazoezi ya pamoja na wenzangu ninamatumaini kupitia Program za mazoezi ambazo ninaendelea nazo nitarejea nikiwa bora zaidi.” amesema Diara
Diara aliitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Mali kinachojiandaa na Mchezo wa Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Zambia utakaopigwa leo Ijumaa, katika Uwanja wa Du 26 Mars nchini Mali.
Kwa mara ya mwisho Diara aliitumikia Young Africans kwenye mchezo wa Mkondo wa Pili wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Zalan FC, lakini alilazimika kutolewa kupindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Aboutwalib Msheri.