Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pape Ousmane Sakho atakuwa sehemu ya msafara wa kuelekea Angola, baada ya kurejea jijini Dar es salaam akitokea kwao, alipokua amekwenda kwa sababu za kifamilia.

Kiungo huyo alitumia muda wa Mapumziko ya Ligi Kuu kurejea nyumbani kwao, kukabilana na changamoto ambazo zilimkumba kupitia familia yake.

Taarifa kutoka Simba SC zimeeleza kuwa Sakho amerejea akiwa salama na atakuwa sehemu ya msafara utakaoelekea Angola Jumamosi (Oktoba 08) tayari kwa mchezo wa Ligi ya Maingwa Barani Afrika dhidi ya Premeiro De Agosto.

Sakho alikosa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji FC uliopigwa Jumapili (Oktoba 02) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ambao ulimalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa 3-0.

Pia hakuwa sehemu ya kikosi kilichokwenda Zanzibar, kwa ajili ya michezo ya Kirafiki dhidi ya Kipanga FC na Malindi SC iliyopigwa wakati wa Kalenda ya FIFA mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mbwana Samatta achomoza kikosi bora Afrika
Mafuta yashuka bei, Watanzania wapata ahueni