Baada ya kukatisha maisha ya watu watatu, akiwemo Kevin Otieno, aliyepigwa risasi 36 katika eneo la Mihang’o lililopo Utawala jijini Nairobi, watu hao wenye silaha wanadaiwa kufika katika mgahawa uliopo kituo cha mafuta cha Njiru, na kuagiza chakula bila hofu wala kuonesha dalili kuwa walifanya tukio la mauaji.
Wengine wawili, waliouawa ni David Ochieng Odera na rafiki yake ambaye hakujulikana mara moja ambapo mmoja wa wahudumu anasema aliona gari aina ya Toyota Land Cruiser jioni ya Septemba 23, lakini hakuitilia maanani na kusema “Hiyo haikuwa mara ya kwanza gari hilo kufika hapa.”
Mhudumu mwingine, alipoonyeshwa picha za gari hilo, alisema aliliona mara kadhaa karibu na Njiru na kuongeza kuwa, “mimi huwa naona gari hili likizunguka hapa,” maelezo aliyoyatoa wakati wauaji hao wakidaiwa kufika kwenye mgahawa huo baada ya kumtupa Bi. Evelyn Nduku, almaarufu Bree, mpenzi wa marehemu Otieno wa Chokaa, Embakasi.
Katika video, iliyonaswa eneo ambalo Otieno aliuawa kikatili, magari aina ya Land Cruiser nyeupe na Toyota Hilux ya kijivu yalionekana yakiwa yameegeshwa huku watu wenye silaha wakimpiga risasi, lakini haikujulikana mara moja ile Hilux ilielekea wapi wakati wapiganaji hao wakila chakula mgahawani.
Watu hao wenye silaha, walitawala vichwa vya habari kwenye mitandao ya kijamii kwa video na picha za kwanza kuvuja wiki mbili zilizopita wakionekana katika nyumba ya Odhiambo na kutoka naye baada ya kumfunga pingu kisha kuondoka naye kumfuata mpenzi wake eneo la China Plaza na kumfunika kitambaa usoni.
Bada ya tukio hilo, mharamia maarufu wa uhalifu anayejulikana kama Lone Survivor, aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa alikuwa ameonywa mara kwa mara Odhiambo lakini alikataa kubadili njia zake akisema “Hata nilimpigia simu binafsi na hakuwahi kusikiliza chochote. Nilikuwa nimemwambia.” na tayari Mkuu wa polisi katika kaunti ndogo ya Kayole, Paul Wambugu, amesema, wanachunguza tukio hilo hilo.