Saa chache baada ya Kikosi cha Azam FC kuwasili Benghazi-Libya tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Kocha Mkuu wa Wababe hao wa Chamazi Denis Lavagne amesema wana kazi kubwa ya kufanya ugenini.

Azam FC iliondoka jijini Dar es salaam jana Alhamis (Oktoba 06) Alfariji kuelekea Libya, huku ikitarajiwa kucheza mchezo wa kwanza kimataifa msimu huu.

Kocha huyo amesema: “Utamaduni wa soka la Afrika kwa kiasi kikubwa unafanana, katika michuano hii kila timu inahitaji kushinda inapocheza nyumbani kwake, na Al Akhdar wapo hivyo pia.”

“Sio timu ya kubeza, nimebahatika kuwaona wakicheza, kwa kweli wana kikosi kizuri, lakini wachezaji wangu watatakiwa kupambana ili wapate matokeo hapa Libya, ili kazi iwe rahisi tutakapocheza nyumbani Dar es salaam.”

“Ninajuwa mchezo utakua mgumu sana hapa ugenini, lakini silaha yangu kubwa ni kuwasisitiza wachezaji wangu wapambane ili kuyashinda majaribu watakayokutana nayo ndani ya Uwanja, tumejiandaa vizuri na ninaamini itakua vile tunavyotarajia.” amesema Kocha huyo kutoka nchini Ufaransa

Azam FC itachza kesho Jumamosi (Oktoba 08) katika Uwanja wa Omar Mukhtar majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Singida Big Stars, Tanzania Prisons zafungiwa
Simba SC kuziba nafasi ya Dejan Georgejevic