Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefungua maonesho ya tatu ya Viwanda na Biashara Mkoa wa Pwani.

Mara baada ya kufungua maonesho hayo, Dkt. Kikwete alitembelea banda la Mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF), ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa jamii, Masha Mshomba alimpa maelezo juu ya huduma zitolewazo na NSSF.

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya huduma zitolewazo na mfukowa hifadhi ya jamii, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,, Masha Mshomba.

NSSF, inashiriki Maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kueleza fursa mbalimbali za Uwekezaji, kutatua kero za wanachama na kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Maonesho hayo, yanaendelea katika stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani, na yatafikia kilele chake Oktoba 10, 2022.

Try Again ahimiza umoja, mshikamano Simba SC
Ruto kuteta na watanzania