Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, imemtangaza Jenerari mpya wa Jeshi la nchi hiyo Sergey Surovikin ama Jen Armageddon, ambaye amekuwa akiongoza kundi la Kusini la wanajeshi nchini Ukraine na Donbass, atachukua uongozi wa jumla wa vikosi vya Urusi.

Jenerali huyo mkongwe, ameshikilia wadhifa wa kamanda wa Kikosi cha Wana anga wa Urusi tangu 2017, ambapo mwaka huo huo, alitunukiwa jina la shujaa wa Urusi kwa jukumu lake katika operesheni ya kijeshi nchini Syria, pia alishiriki katika Operesheni huko Chechnya.

“Kwa uamuzi wa Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Urusi, Jenerali wa Jeshi Sergey Surovikin aliteuliwa kuwa kamanda wa kikundi cha pamoja cha vikosi katika eneo la operesheni maalum ya kijeshi,” ilisema taarifa ya wizara hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za vyombo vya habari, Surovikin alipewa jina la utani la ‘Jenerali Armageddon’ na wenzake, wakitaja mtazamo wake mkali na usio wa kawaida wa operesheni za kijeshi ambapo Surovikin alichukua jukumu la kikundi cha Kusini wakati wa kampeni ya kijeshi ya Moscow huko Ukraine.

Mwishoni mwa mwezi Juni 2022, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilidai kwamba wanajeshi wake walikuwa wameondoa kikosi kikubwa cha Ukraine kilichozingirwa katika eneo la Gorskoye, katika Jamhuri ya Watu wa Lugansk.

Fei Toto ambwaga Moses Phiri, Reliants Lusajo
Azam FC kuwasili leo kujipanga upya