Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss amemfuta kazi Waziri wake wa Fedha, Kwasi Kwarteng muda mfupi kabla ya kiongozi huyo kupanga kuachana na hatua za kiuchumi katika jitihada za kujinusuru na misukosuko ya kisiasa inayoikabili nchi hiyo.

Truss, aliye madarakani kwa siku 37 pekee, anatathmini upya hatua za punguzo la ushuru zilizosababisha ongezeko la gharama za ukopaji, na kuilazimu Benki Kuu ya Uingereza kuingilia kati.

Kufuatia utenguzi huo, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Jeremy Hunt, ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Fedha kujaza nafasi ya Kwarteng.

Hata hivyo, bado haijafahamika ikiwa kufutwa kazi kwa waziri huyo wa fedha kunaweza kumnusuru Truss na shinikizo kubwa dhidi yake, akilaumiwa kuwa kigeugeu kwenye utawala wake.

Rais atoa angalizo kwa jamii ugonjwa wa Ebola
Polisi waongeza ujuzi mawasiliano kukabiliana na majanga