Serikali ya nchi ya Kenya, imekanusha madai kuwa haikulipa riba iliyotokana na mkopo uliotolewa na Serikali ya China, kwa ajili ya ujenzi wa njia ya reli ya kisasa (SGR), kutoka bandari ya Mombasa iliyofunguliwa mwaka 2017.

Mradi huo wenye thamani ya dola bilioni 5, ulifadhiliwa kwa asilimia 90 na Uchina, ukichukua nafasi ya kile kinachojulikana kama “Lunatic Express” mstari uliojengwa zaidi ya karne moja na mamlaka ya kikoloni ya Uingereza, ambayo ilikuwa maarufu kwa ucheleweshaji wa muda na uharibikaji.

Gazeti la Business Daily la Kenya liliripoti kuwa serikali ilishindwa kulipa riba ya mkopo huo katika mwaka wa fedha ulioishia Juni, na hivyo kuvutia faini ya shilingi bilioni 1.312 za Kenya ambazo ni sawa na dola za kimarekani milioni 10.8.

Waziri wa Hazina, Ukur Yatani aliikataa ripoti hiyo akiita ni taarifa potofu na kuongeza kuwa hali ya kifedha ya shirika lao lenye nguvu ya kiuchumi kwa Afrika Mashariki ni thabiti na imara huku akisema “Tunataka kusema kwa uthabiti kwamba Kenya haijawahi kukiuka majukumu yake ya kulipa madeni kwa wakopeshaji wake yeyote.”

Reli ya Standard Gauge (SGR), ni mradi mkubwa zaidi wa miundombinu nchini Kenya tangu ijipatie uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1963, na ulizinduliwa kama mpango mkuu na viongozi wa Afrika Mashariki kuunganisha mataifa yao kwa njia ya reli.

Reli hiyo, ilipaswa kusimamiwa na mwanakandarasi wa China kwa miaka mitano kabla ya kukabidhiwa kwa serikali ya Kenya, lakini imeleta hasara, huku wachanganuzi wakihofia hali hiyo huenda ikaendelea baada ya Rais William Ruto mwezi uliopita kutengua sera iliyoweka lazima kwa mizigo kwa kutumia reli.

Bilioni 2.2 wakabiliwa na uoni hafifu, upofu Duniani
Waganda walia na Museveni sheria mpya ya mtandao