Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amewatembelea Wazee katika maeneo tofauti ya mkoa wa mjini magharibi, kwa lengo la kuwajulia hali na kuwafariji wale wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali ya uzeeni.

Othman, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo Zanzibar, amewatembelea Wazee hao ikiwa ni sehemu ya ziara maalumu ya kuwatembelea na kuwajulia hali na kuwafariji wagonjwa na wazee.

Akiwa eneo hilo, amesema wazee ni hazina kubwa na muhimu na unapowatembelea unajifunza mambo mbalimbali waliyopitia ambayo ni muhimu katika kuongeza maarifa yatakayokujenga na kukuimarisha kimaisha.

Amesema, anawaombea wagonjwa hao aliowatembelea kuendelea kuwa na subira na kuwatakia dua kwa Mwenye enzi MUNGU, ili wapone haraka na pia kuwatakia maisha marefu na yenye afya njema.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman (kushoto), akizungumza na Wazee, alipowatembelea mjini Unguja, hii leo Oktoba15, 2022.

Wakiongea baada ya kupokea ugeni huo, baadhi ya wazee wamemshukuru Othman kwa kuwatembelea na kumshauri kuendeleza tabia hiyo kwa kuwa ni jambo jema lenye kuleta mshikamano kwa Taifa.

Katika zaiara hiyo, Othman alitembelea baadhi ya wagonjwa na wazee katika mitaa wa Shangani, Micheznzani, Mfenesi Mazizi, Magomeni Wilaya ya mjini Unguja, Munduli Magharibi ‘A’ na Mwanakwerekwe Jitimai, Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja.

Rais Samia azindua kituo cha kupokea na kupoza umeme
Idadi ya vifo mlipuko mgodini yafikia 40