Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametembelea na kufanya sala kwenye Kaburi la Kaburi la Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Rais Samia ametembelea aneo hilo hii leo Oktoba 15, 2022 ambapo pia alipata wasaa wa kutembelea makumbusho ya Rais huyo ambaye alifariki majira ya saa 12:00 jioni kutokana na tatizo la moyo,  Machi 17, 2021.

Magufuli alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliokuwa hawaamini uwepo wa ugonjwa wa Uviko-19, ambapo mwaka 2020 alisema Tanzania ilifanikiwa kupambana na kuudhibiti ugonjwa huo kupitia siku tatu za maombi. 

Hata hivyo, Magufuli atakumbukwa kwa mengi hasa kutokana na juhudi alizofanya katika kuleta maendeleo Tanzania ndani ya muda mfupi wa utawala wake.

   Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 16, 2022   
Majaliwa 'aipa tano' Kagera Sugar kuongeza uzalishaji wa Sukari