Mashirika ya Umoja wa Mataifa kupitia Mradi wa Pamoja wa Kigoma KJP, yameendelea kutekeleza kwa vitendo azma ya malengo ya maendeleo endelevu namba moja la kutokomeza umaskini kwa kushirikisha wananchi kwenye miradi ya kuwawezesha kuinua vipato.

Mradi huo wa KJP, ulioanza mwaka 2017 Mkoani Kigoma hivi karibuni ulifanikisha maonesho kwenye Halmashauri ya Mji wa Kasulu, maonesho yaliyoleta wanufaika wa miradi ya KJP kutoka wilaya za kasulu vijijini, Kakonko na Kibondo.

Miongoni mwa wanufaika wa mradi huo, ni kijana Levis Rugayaza ambaye licha ya kuwa ni mwanafunzi anashirikiana na baba yake kufuga samaki kufuatia mafunzo ya ufugaji bora kupitia mradi wa pamoja wa Kigoma.

Levis anasema, “sisi tunafuga samaki kwa ajili ya kujipatia kipato lakini pia kuongeza aina mbalimbali za lishe katika kaya yetu ikiwemo protini. Tunajipatia mboga mboga kama samaki.”

Kilimo, kazi ambayo inatajwa kuwainua wakulima wengi Duniani.

Katika maonesho hayo, alionesha bwawa la mfano likiwa na samaki ambamo amechanganya kambale na sato akisema kambale wanasaidia kuchimba mashimo ambayo yatamsaidia sato kutaga mayai yake na wakati wa kiangazi, maji yakipungua sato atatumia mashimo hayo kujificha ili kukwepa joto linalotokana na jua.

Kijana huyo, pia ametoa ujumbe kwa vijana hususan walio shuleni akisema, ujumbe wangu si kwa walio shuleni tu na hata wale wasio shuleni ya kwamba wajishughulishe na kazi mbalimbali kwa sababu kilimo huwainua watu ikiwemo wafugaji wa samaki.

Uchumi wa Wanawake Vijijini kuimarishwa
Simba SC yaanza kuiwinda Young Africans