Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma kutimiza wajibu wao kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anataraji watumike baada ya kuwateua.

Majaliwa, ametoa wito huo hii leo Oktoba 19, 2022 wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa, Wilaya na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kwenye ukumbi wao mara baada ya kuzindua jengo la Halmashauri hiyo.

Amesema, “Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona watumishi wa umma mkiwatumikia Watanzania. Nenda kwa wananchi mkawasikilize. Huwezi kuwahudumia bila kuwasikiliza na huwezi kujua changamoto zao bila kuwasikiliza.”

Aidha, amewataka viongozi na watumishi hao wafanye kazi kwa matokeo chanya, kufuata maelekezo na kuzingatia nidhamu na kusema, “Tuna fedha za ndani na za Serikali Kuu, tuzisimamie vizuri na naomba msijiingize kwenye matumizi mabaya.”

Kuhusu hoja za CAG, Waziri Mkuu amesema Halmashauri hiyo ya Wilaya ilikuwa na hoja 46 ambapo hoja 28 zimefungwa na hoja 18 bado hazijafungwa huku akiwataka kumalizia hoja 18 zilizobakia.

Kuhusu ujenzi wa hospitali ya Halmashauri hiyo, Waziri Mkuu amewataka wakamilishe ujenzi kwa viwango alivyoviona na akampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Sajidu Mohammed kwa usimamizi mzuri.

Mapigano yapamba moto, wananchi wasema wanamuachia Mungu
Makahaba waitaka Mahakama itende haki mauaji ya wenzao sita