Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi, Caroline Kitana Chipeta amewasilisha hati za utambulisho kwa Mfalme Willem-Alexander wa Uholanzi katika hafla iliyofanyika kwenye Kasri za Kifalme iliyoko Noordeinde, The Hague, nchini humo.
Uwasilishaji huo wa hati, unafuatia hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kumteua Caroline Kitana Chipeta, kuwa Balozi wa Tanzania katika Falme ya Uholanzi mapema.