Ukraine inathibiti matumizi ya umeme kama sehemu ya kujibu mashambulizi ya Urusi kwenye miundombinu ya nishati, ambayo yamezua hofu kuhusu jinsi nchi hiyo iliyokumbwa na vita itakavyojimudu wakati wa msimu wa baridi kali.

Kampuni ya kitaifa ya nishati Ukrenergo, imewaambia raia wa nchi hiyo kuchaji simu na betri, na kuhakikisha wana tochi tayari, kabla ya kuanza kukatizwa kwa umeme kuanzia leo Oktoba 20, 2022 kwa muda wa masaa manne.

Katika hotuba yake ya jioni kwa taifa, rais wa nchi hiyo Voldodymr Zelensky amesema kwamba kuna uharibifu mpya wa miundombinu muhimu na kwamba leo, vituo vitatu vya nishati viliharibiwa na adui.

Zelensky amesema watafanya kila linalowezekana kurejesha uwezo wa kawaida wa nishati nchini humo. Ili kupunguza kukatika kwa umeme, watu wamehimizwa kutumia umeme kidogo iwezekanavyo kati ya saa moja asubuhi na saa nne usiku.

Ongezeko la majanga: Serikali yatangaza hali ya hatari
Ukali wa maisha: Waziri Mkuu atangaza kujiuzulu