Wazazi na walezi, wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha na kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu, na badala yake watumie vituo vya utayari 36 ambavyo vimeanzishwa kuwaandikisha ili wapate elimu ya awali itakayowaandaa kujiunga na darasa la kwanza mwaka 2023.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu Mkoa wa Pwani, Bi. Sara Mlaki wakati wa kufunga Mafunzo ya siku Tano Kwa Walimu Jamiii Wasaidizi(MJM) wapatao 38 kutoka halmashauri zote tisa zilizopo katika Mkoa wa Pwani yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kufundisha watoto wenye umri wa miaka 5-9.
Amesema, watoto ambao ni walemavu na wamefikia umri wa kuanza shule ya awali wanapaswa kupatiwa haki zao za msingi, kama ilivyo kwa watoto wengine kwa kupatiwa elimu bila ya ubaguzi.
Aidha, Bi. Mlaki pia amewaasa walimu Jamiii Wasaidizi (MJM), ambao wemepatiwa mafunzo hayo kwa namna ya kipekee kwa kuwatete watoto wenye ulemavu ili wasibaguliwe na kuhakikisha wanapatiwa haki zao za kimsingi.