Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa chini ya Umri wa Miaka 23, Hemed Seleman Morocco amesema kikosi chake kimekamilisha maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko wa Pili wa Kuwaniwa Kufuzu Fainali Afrika (AFCON U23).
Tanzania itakua mwenyeji wa Nigeria kesho Jumaosi (Oktoba 22) dhidi ya Nigeria, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Kocha Morocco amesema kutokana na maandalizi walioyafanya ana uhakika kikosi chake kitakwenda kupambana kwenye mchezo huo, ili kupata matokeo katika Uwanja wa nyumbani.
“Wachezaji wapo tayari, wengi wamesharipoti kambini na wapo FIT, jambo zuri walipita katika timu za miaka 17 na 20 ambazo ni sehemu sahihi kwa vijana, Wachezaji wangu wananipa moyo.” Amesema Kocha Morocco ambaye aliwahi kuzinoa klabu za Coastal Union, Namungo FC na Timu za taifa za Taifa Stars na Zanzibar Heroes.
Kuhusu wapinznai wao Nigeria, Morocco amesema anawafahamu vizuri na wana kikosi imara ambacho kinaweza kumpa ushindani wa kweli ndani ya dakika 90.
Amesema kutoana na kufahamu hilo, amekiandaa kikosi chake kukabiliana na changamoto zozote ambazo zitajitokeza kwenye mchezo huo, ili kufikia lengo la kushinda nyumbani kabla ya kwenda ugenini Nigeria.
Mshindi wa Jumla katika mchezo huo atatinga katika Mzunguuko watatu na wa mwisho wa kuwania nafasi saba za kwenda nchini Morocco kushiriki AFCON U23, ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2024.