Mwanahabari wa Pakistani na mtangazaji wa TV Arshad Sharif amepigwa risasi na kufariki  usiku wa Octoba 23, 2022, katika kaunti ya Kajiado, Jirani na mji mkuu Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, Sharif alipigwa risasi kichwani na kuuawa kwenye kizuizi cha barabarani katika barabara kuu ya Nairobi-Magadi katika tukio la utambulisho kimakosa.

Dereva wake ambaye pia alijeruhiwa katika tukio hilo, walikuwa wakiendesha gari kutoka mji wa Magadi kuelekea Nairobi walipopigwa alama kwenye kizuizi cha barabarani kilichokuwa na kundi la maafisa wa polisi.

Hata hivyo, Polisi nchini humo wamethibitisha kuanza uchunguzi dhidi ya mauaji ya mwanahabari huyo raia wa Pakistani Arshad Sharif aliyeuawa kwa kupigwa risasi.

Msemaji wa Polisi Bruno Shioso anasema wanachunguza hali iliyosababisha kifo cha mwanahabari huyo Arshad Sharif.

Cameroon: Mafuriko yatatiza maisha
Azam FC yafafanua kuwabakisha Simba SC Kwa Mkapa