Mji wa soko wa Kousseri katika Jimbo la Kaskazini mwa Cameroon, karibu na mpaka na Chad, umekuwa ukikabiliwa na mafuriko makubwa kwa wiki moja.
Mito miwili ya kikanda yenye muunganiko wake, Logone na Chari, na yote inaviwango vya juu vya maji amabyo yanatabiriwa kuongezeka zadi.
Mifuko ya mchanga iliyokuwa ikitumiwa katika jaribio la kuzuia mito, lakini kwa sehemu nyingi za Kousseri ilikuwa tayari imechelewa.
Nyumba katika mji huo zimefurika na watu wameonekana wakitembea kwenye maji yenye matope hadi magotini, wakiwa wamebeba mali kujaribu kuziokoa kutokana na mafuriko.
Familia zimeachwa bila makao na zimejenga makazi ya muda kutoka kwa vijiti na shuka kwenye sehemu kavu ya juu. “Niko katika matatizo makubwa,” alimwambia mkazi wa Kousseri Bouba Vira, ambaye familia yake imelazimika kutelekeza nyumba yao.
Mvua kubwa ilisababisha uharibifu mkubwa mwezi Agosti, na tena hali imekuwa mbaya kutokana na kuongezeka kwa maji ya mafuriko.
Mito ya Logone na Chari hutenganisha Cameroon na nchi jirani ya Chad ambayo ilitangaza hali ya hatari wiki hii kusaidia kukabiliana na mgogoro huo.