Vikosi vya usalama vya Rwanda, vilivyo katika operesheni za kukabiliana na ugaidi jimbo la kaskazini mwa Msumbiji la Cabo Delgado, kwa mara ya pili vimegundua hifadhi ya silaha iliyoachwa na wanajihadi.

Silaha hizo, zimekutwa katika msitu wa Limala uliopo Wilaya ya Mocimboa da Praia ambayo ilikuwa ni ngome ya wanajihadi kabla ya kusambaratishwa na muungano wa Jeshi la Msumbiji na Rwanda, Agosti 2021.

Wizara ya Ulinzi ya Rwanda, imesema waasi hao wa Kiislamu wanaohusishwa na kundi la Islamic State, walijaribu mara kadhaa kurejea eneo hilo kuchukua silaha zao, lakini hawakufanikiwa.

Wanajihadi hao, walifukuzwa kutoka maeneo hayo ya Wilaya mbili za Palma na Mocímboa da Praia, zilizo chini ya jukumu la vikosi vya usalama vya Rwanda, lakini bado wamesalia katika Wilaya zilizo jirani.

Mohamed Ouattara aomba kuondoka Simba SC
Sunak apewa mbinu kuimarisha uchumi