Matokeo ya tafiti iliyofanywa nchini, yanaonesha kati ya Watanzania 100, watu tisa kati yao wanaishi na Ugonjwa wa Kisukari, kutokana na ongezeko la ugonjwa huo kwa kila mwaka.

Mwenyekiti wa Chama cha Kisukari Tanzania (TDA), Prof. Andrew Swai amesema waathiriwa wa magonjwa yasiyoambukiza wanaongezeka kila Mwaka kutokana na mtindo mbaya wa maisha.

Miguu iliyovimba.

Amesema, wagonjwa hao wamekuwa wakijikluta na tatizo hilo kwa kutozingatia mpangilio wa vyakula, pamoja na kutojishuhulisha na jambo lolote ikiwemo kukosa kufanya mazoezi.

Kisukari ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu na sababu yake ni kuwa na uhaba wa homoni ya insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali insulini, ukiwa na dalili za kukojoa kupita kiasi kiu kubwa, kuona vibaya, matatizo ya macho na kipofu, kuchoka haraka na vidonda visivyopona haraka na kuvimba miguu.

China yasamehe baadhi ya madeni ya Tanzania
Viongozi wa Dini wakosolewa hadharani