Kiungo Mtanzania Mzamiru Yassin ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi OKTOBA wa Simba SC akiwashinda Beki Joash Onyango pamoja na Kiungo Mshambuliaji Augustine Okrah.

Mzamiru ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa kupigiwa kura nyingi na Mashabiki wa Simba SC, kupitia Tovuti ya Klabu hiyo.

Simba SC imethibitisha na kumtanzania Kiungo huyo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii: Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Oktoba inakwenda kwa Mzamiru Yassin.

Hongera kiungo punda? #NguvuMoja

Asakwa kwa mauaji ya mpenzi wake, kuchoma nyumba
Kocha Mgunda aiwinda Singida Big Stars kiaina