Kikosi cha Young Africans kiondoka jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Novemba 04) kuelekea Tunis-Tunisia kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili hatua ya Mtoano Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Young Africans itacheza ugenini Jumatano (Novemba 09), ikiwa na deni la kusaka ushindi wa aina yoyote au sare ya mabao ili itinge Hatua ya Makundi.
Mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi Jumatano (Novemba 02), ulishuhudia Young Africans ikiambulia sare ya bila kufungana.