Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema mapigano makali zaidi nchini humo kwa sasa yamejikita katika mji wa Donbass karibu na miji ya Bakhmut na Soledar katika mkoa wa Donetsk huku akisema wao wanaendelea vyema.
Katika kipindi hiki, ambacho Urusi ikiwa katika mpango wake wa kuongeza wanajeshi wa akiba zaidi ya 300,000 kwa ajili ya kufanikisha vyema uvamizi wake katika maeneo hayo, Zelensky anasema wapo katika udhibiti.
Amesema Urusi tayari imepoteza maelfu ya wanajeshi wake katika eneo hilo ambapo kwa mara nyingine Zelensky amesisitiza kwamba, Ukraine itapigana hadi ifanikishe kuirejesha kwa ukamilifu mipaka yake ya asili.
Haya yanajiri, wakati ambapo hivi majuzi Volodymyr Zelensky alisema mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu ya nishati imewaacha takriban watu milioni 4.5 bila umeme.