Rais wa Marekani Joe Biden na washirika wake, wamewahimiza kwa faragha viongozi wa Ukraine kuonesha nia ya kufanya mazungumzo na Urusi na kufutilia mbali msimamo wao wa kutojihusisha na mazungumzo ya amani iwapo Rais Vladmir Putin hataondolewa madarakani.
Licha ya kwamba jambo hilo halijawekwa wazi, lakini watu ambao hawakutajwa majina wanaofahamu kuhusu mazungumzo hayo wamenukuliwa wakisema ombi la maafisa wa Marekani halikulenga kuisukuma Ukraine kwenye meza ya mazungumzo.
Aidha, hatua hiyo inatajwa kama jaribio lililopangwa la kuhakikisha Ukraine inadumisha msaada wa mataifa mengine yanayohofia kuchochea vita vya muda mrefu na Baraza la Usalama wa Marekani halikujibu haraka lilipoulizwa iwapo ripoti hiyo iwapo ni sahihi.
Hata hivyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani aliongea kuwa kwasasa watasema kwa vitendo na sauti kubwa kuliko maneno, na kwamba iwapo Urusi iko tayari kwa mazungumzo, inapaswa kusimamisha mashambulizi ya mabomu na makombora na kuondoa vikosi vyake nchini Ukraine.