Kampuni ya mawasiliano ya mtandao ya Twitter, imezindua mfumo mpya wenye utata wa malipo ya usajili ambao mmiliki mpya wa kampuni hiyo, Elon Musk, aliwaagiza wafanyakazi wake kuunda baada ya kuchukuwa udhibiti wa kampuni hiyo wiki iliyopita.

Uzinduzi huo uliofanyika hapo jana Novemba 5, 2022 utaanza kuwaruhusu watumiaji kujiandikisha kwenye toleo jipya la Twitter Blue, ambalo Musk amesema litagharimu dola 8 kwa mwezi, na kutazamiwa kuwapa watumiaji alama ya buluu na manufaa ya kupungua kwa matangazo katika kurasa zao za mtandao huo.

Alama ya biashara ya mtandao huo maarufu wa kijamii.

Musk, alichukua umiliki na udhibiti wa kampuni hiyo ambayo ni jukwaa linaloongoza duniani kwa mijadala na uanaharakati, huku ahadi na kauli zake zikisababisha wasiwasi, likiwemo onyo kutoka kwa Umoja wa Mataifa na ombi la msamaha kutoka kwa mwanzilishi mwenza wa Twitter.

Mpaka sasa, bado hakuna wadau waliojitokeza kuzungumzia hatua hiyo, ingawa wadadisi wa mambo wanasema huenda bado wanatafakari ili kuja na hoja mahususi za kumshauri mmiliki huyo mpya kama sehemu ya maboresho ambayo hayatakuwa na athari kwa pande zote.

DRC na Rwanda zajadili kupunguza mvutano
Marekani yaishauri Ukraine 'kuomba poo' vita na Urusi