Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa taasisi za dini nchini kuendelea kuiunga mkono Serikali katika utoaji wa huduma za jamii, hususan katika kipindi hiki ambacho imewekeza katika miundombinu bora ya afya, elimu na maji.

Mjaliwa, ameyasema hayo hii leo Novemba 06, 2022 wakati wa ibada maalum ya kusimikwa kwa askofu mteule wa kanisa la baptist Tanzania, Askofu Arnold Manase Mollel na viongozi waandamizi katika viwanja vya seminari vilivyopo Ngaramtoni, Mkoani Arusha.

Amesema, Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora, nafuu na kwa wakati katika maeneo mbalimbali nchini, na kuongeza kuwa wataendela kuboresha miundombinu ya elimu, afya na maji ili kuhakikisha watanzania wote wanapatiwa huduma za kijamii.

Kambi ya wakimbizi yashambiliwa, Watano wauawa

“Ninapenda niwahakikishie kwamba Serikali kwa upande wake imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu, afya na maji katika kuhakikisha watanzania wote bila kujali dini zao, rangi zao au itikadi zao wanahudumiwa ipasavyo” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu, amesema kuwa Serikali imeongeza fedha za kusomesha wataalamu bingwa na bobezi katika sekta ya afya hadi kufikia shilingi bilioni 8 kutoka shilingi bilioni 3 za mwaka wa fedha 2021/2022. ambapo ameongeza kuwa “Hii itasaidia kuboresha huduma kwa wananchi na kupunguza rufaa za nje ya nchi.”

Aidha, amezipongeza Taasisi za dini ikiwemo kanisa la Wabaptist wa Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwaongoza watu na kutatua shida zao za kijamii, ikiwemo kuwapa mafundisho ya kiroho, kutoa ushauri na kuwajenga kiimani.

Amesema, “Kwa mfano, katika jumla ya shule za Msingi 19,261 zilizopo nchini, sekta binafsi na taasisi za dini zinamiliki shule zipatazo 2,080. Kwa upande wa Shule za Sekondari 5,540, shule 1,329 ni za Sekta Binafsi na Taasisi za Dini”

Aidha, amempongeza Baba askofu Anorld Manase Mollel kwa kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Wabaptist na kumuombea heri katika utimizaji wake wa majukumu ya kuwaongoza Kanisa na waumini.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 7, 2022 
Teachers Junction wavunja ukimya mkanganyiko taarifa za Walimu