Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa, (Masuala ya mabadiliko ya Tabianchi), Simon Stiell amesema hawezi kuwa mlezi wa kurejea nyuma katika lengo la kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa asilimia 45 kufikia mwaka 2030.

Stiell, ameyasema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP27, unaofanyika nchini Misri kwa siku 13 kunzia Novemba 6, 2022.

Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa, (Masuala ya mabadiliko ya Tabianchi), Simon Stiell. Picha ya Daily World.

Amesema, lengo la utoaji huo wa hewa chafu ni kupunguza ongezeko la joto duniani kwa nyuzi joto 1.5 zaidi ya viwango vya mwishoni mwa karne ya 19 na kudai kuwa watawawajibisha watu iwe ni Marais, Mawaziri Wakuu ama Wakurugenzi.

COP27, imeanza kwa kutoa tahadhari juu ya kurudi nyuma kwa juhudi za kupunguza hewa chafu, na wito kwa mataifa tajiri kufidia nchi maskini baada ya mwaka mmoja wa majanga mabaya ya hali ya hewa.

Mwamnyeto aahidi makubwa Tunisia
Simba Queens kuwavaa mabingwa wa Afrika