Klabu ya FC Barcelona itaanzia nyumbani Camp Nou katika mchezo wa Hatua ya Mchujo ya Michauno ya Europa League ikipangwa na Manchester United ya England.

Miamba hiyo ya Hispania iliangukia kwenye mchezo huo wa Hatua ya Mchujo, baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi C, kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu huu 2022/23.

Machester United nao wamekumbana na FC Barcelona baada ya kupangwa kwa Droo ya Europa League, kufuatia kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Msimamo wa Kundi E, katika michuano hiyo.

Mchezo wa Mkondo wa Kwanza kati ya miamba hiyo utachezwa Februari 16 kwenye Uwanja wa Camp Nou, huku mchezo wa Mkondo wa Pili ukipangwa kuunguruma Februari 23 katika Uwanja wa Old Traffold.

Michezo mingine ya hatua ya mchujo ya Europa League iliyopangwa katika leo Jumatatu (Novemba 07) Mchana mjini Nyon nchini Uswiz.

Juventus (Italy) Vs Nantes (Ufaransa)

Sporting CP (Ureno) Vs Midtjylland (Denmark)

Shakhtar Donetsk (Ukraine) Vs Rennes (Ufaransa)

Ajax (Uholanzi) Vs Union Berlin (Ujerumani)

Bayer Leverkusen (Ujerumani) Vs AS Monaco (Ufaransa)

Sevilla (Hispania) Vs PSV Eindhoven (Uholanzi)

Red Bull Salzburg (Austria) Vs AS Roma (Italia)

Michezo ya Mkondo wa Kwanza imepangwa kucheza Februari 16 na michezo ya Mkondo wa Pili umepangwa kuunguruma Februari 23.

Kigwangala 'amshukia' Mkenda, Spika aingilia kati
Rais aagiza Kijana aliyeokoa watu 24 kupewa ajira Jeshini