Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamechanga zaidi ya shilingi milioni tano kwa ajili ya kumpa kijana Majaliwa Jackson, kama pongeza kwa ushujaa aliouonesha kwa kuwaokoa watu 24 kwenye ajali ya ndege ya Precision Air, Novemba 6, 2022.

Kuchangwa kwa fedha hizo kumetokana na Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla kuomba mwongozo wa Spika endapo wabunge wanaweza kufanya jambo hiklo kwa ajili ya kutambua mchango wa Majaliwa.

Ndege iliyopata ajali ziwa Victoria.

Majaliwa amefika bungeni jijini Dodoma kufuatia mwaliko wa Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato na Spika wa Bunge Tulia Ackson aliridhia kuchangwa kwa fedha hizo baada ya maelekezo kutolewa.

Ndege ya hiyo, yenye namba za usajili 5HPWF iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza ilishindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba na kutua Ziwani mita chache kabla ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba.

Viongozi wa Dini wakataa 'unafiki' wa Jumuiya ya Kimataifa
Afya ya uzazi ni changamoto kwa Mataifa