Hatimaye Klabu ya Ashton United inayoshiriki Ligi Daraja la 7 nchini England, imefanikiwa kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Norway na Klabu ya Manchester City Erling Haaland.

Klabu ya Ashton ilijinasibu kuwa tayari kumsajili Mshambuliaji huyo mwanzoni mwa juma hili huku ikiamini ingeweza kumpata kwa kigezo cha Fainali za Kombe la Dunia, ambapo Haaland hatashiriki kufuatia taifa lake kushindwa kufuzu.

Haaland amejiunga na klabu hiyo kwa Mkataba wa Mkopo wa siku 28, ambazo zitashuhudia Ligi Kuu ya England ikisimama kupisha Fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Jumapili (Novemba 20) nchini QATAR.

Haaland amefikia uamuzi huo kwa ajili ya kujiweka fiti, huku akiamini Ligi Kuu ya England itakaporejea mapema mwaka 2023, atakuwa na uwezo wa kuendelea kuipambania Manchester City.

Erling Haaland aliyeifungu Manchester City mabao 18 katika michezo 13 aliocheza hadi sasa, alisajiliwa Etihad Stadium mwanzoni mwa msimu huu akitokea Borussia Dortmund, kwa ada ya Pauni Milioni 51.2

Ulipaji wa kodi bila shurti ni uzalendo: TRA
Christopher Nkunku kuikosa safari ya QATAR