Kikosi cha Mabingwa wa Dunia ‘Timu ya Taifa ya Ufaransa’ Kimeanza safari ya kuelekea QATAR tayari kwa shughuli ya kutetea ubingwa wake.
Ufaransa imeanza safari hiyo huku ikimkosa Mshambuliaji wake Christopher Nkunku aliyepata majeraha kwenye mazoezi ya mwisho, kufuatia kugongana na Kiungo wa klabu ya Real Madrid Eduardo Camavinga.
Shirikisho la Soka nchini Ufaransa ‘FFF’ limethibitisha taarifa za kuondoka kwa Kikosi cha nchi hiyo kuelekea QATAR, huku kukiwa na matumaini makubwa ya kutetea ubingwa walioutwaa mwaka 2018 nchini Urusi.
Wachezaji wengine ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kwenye Fainali za Mwaka huu 2022 ni Viungo Paul Pogba, N’Golo Kante pamoja na Beki Prisnel Kimpembe.
Kikosi cha Ufaransa kilichoanza safari leo Jumatano (Novemba 16), Walinda Lango ni Hugo Lloris, Steve Mandanda, Alphonse Areola
Mabeki: Benjamin Pavard, Axel Disasi, Raphael Varane, Jules Kounde, William Saliba, Dayot Upamecano, Lucas Hernandez, Theo Hernandez, Ibrahima Konate
Viungo: Matteo Guendouzi, Aurelien Tchouameni, Youssouf Fofana, Adrien Rabiot, Jordan Veretout, Eduardo Camavinga
Washambuliaji: Antoine Griezmann, Olivier Giroud, Kylian Mbappe, Ousmane Dembele, Karim Benzema, Kingsley Coman, Marcus Thuram
Ufaransa inatarajiwa kuanza safari ya kuelekea QATAR leo Jumatano (Novemba 16) tayari kwa Fainali za Kombe la Dunia, huku ikipangwa Kundi D sambamba na timu za mataifa ya Tunisia, Australia na Denmark.
Ufaransa itaanza kampeni ya kutetea Ubingwa wa Dunia Novemba 22 kwa kucheza dhidi ya Australia katika Uwanja wa Al Janoub, uliopo mjini Al Wakrah.
Mchezo wa pili Ufaransa itacheza dhidi ya Denmark Novemba 26 mjini Doha katika Uwanja wa 974 na itamaliza Michezo ya Hatua ya Makundi kwa kupapatuana na Tunisia Novemba 30 mjini Al Rayyan kwenye Uwanja wa Education City.
Timu nyingine zinazotarajiwa kuwasili QATAR kuanzia leo Novemba (16) ni Senegal, Wales, na Argentina
Novemba 17: Saudi Arabia, Germany, Canada, Poland, Mexico
Novemba 18: Belgium, Spain, Japan, Croatia, Ghana, Costa Rica
Novemba 19: Cameroon, Portugal, Serbia, Uruguay, Brazil