Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasridden Mohamed Nabi amefichua siri ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Singida Big Stars, iliyofunga safari kutoka mkoani Singida hadi Dar es salaam.

Young Africans jana Alhamis (Novemba 17) ilikua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa ilicheza mchezo wake wa Kumi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikidhamiria kutetea taji la ubingwa wa ligi hiyo.

Kocha Nabi amesema kujituma na kupambana kwa wachezjai wake ndio siri ya ushindi uliopatikana kwenye chezo huo, ambao ulitabiriwa kuwa na upinzani mkubwa kabla ya kipyenga hakijapulizwa na Mwamuzi Ramadhan Kayoko.

Amesema alichokifanya kabla ya kwenda Uwanjani aliwahimiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma na kutambua umuhimu wa kupata alama tatu za mchezo huo, kitu ambacho kilionekan wakati wote wa dakika 90.

“Niliwahimiza kucheza kwa kujituma na kutambua umuhimu wa sisi kushinda mchezo huo, walipambana na wametupa matokeo yanayoendelea kulinda heshima yetu kama Mabingwa.”

“Jambo kubwa katika ushindi huu ni kuendelea kudhihirisha ubora wa kikosi changu ambacho kina wachezaji wenye umahiri mkubwa, na sasa tunajipanga kwa mchezo ujao ambao pia utakua mgumu.” amesema Kocha Nabi.

Mchezo ujao utashuhudia Young Africans ikisafiri hadi mjini Dodoma kucheza na Dodoma Jiji FC katika Uwanja wa Jamhuri siku ya Jumanne (Novemba 22).

Mayele: Bao la kwanza nimemzawadia Mwanangu
Kelvin Mandla: Simba SC ni kubwa Afrika