Mfumuko wa bei ambao umechangiwa na kudorora kwa ukuaji wa uchumi duniani kwa kuchochewa na vita nchini Ukraine na janga la nishati duniani, kwa pamoja vinasababisha anguko la viwango vya mishahara na ujira kwenye nchi nyingi duniani.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO, imesema janga hilo limepunguza uwezo wa manunuzi wa watu wa vipato vya kati, huku kaya za kipato cha chini zikiathiriwa zaidi.

Ripoti hiyo, ambayo imetolewa jijini Geneva nchini Uswisi imepatiwa jina la Ripoti ya Ujira duniani mwaka 2022-2023 ikiwa na mnyumbulisho wa athari za mfumuko wa bei na maradhi ya Uviko-19 kwenye ujira na uwezo wa ununuzi.

Wafanyabiashara wakiwa mawindoni.

Aidha, ripoti hiyo pia inakadiria kuwa kiwango cha ujira duniani kimepungua kwa asilimia hasi 0.9 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2022, ikiwa ni mara ya kwanza katika karne hii ambapo kiwango cha ujira kimekuwa hasi.

Kwa upande wa kundi tajiri la nchi 20, G20, ujira halisi ulipungua kwa asilimia hasi 2.2 huku nchi 20 zinazoibuka kiuchumi, ujira halisi ukiwa ni asilimia 0.8, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 2.6 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Gilbert Houngbo amesema uwepo wa majanga yanayokabili dunia yamechochea kuporomoka kwa ujira halisi na kwamba ukosefu wa usawa kwenye kipato na umaskini vitaongezeka iwapo uwezo wa ununuzi kwa wale wanaopata kipato cha chini hautashughulikiwa.

Rais Samia aongoza maadhimisho siku ya Ukimwi
Serikali yataka elimu ya Bima kwa jamii