Rais wa Rwanda, Paul Kagame amemtuhumu Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Felix Tshisekedi kutumia migogoro ya mashariki mwa nchi yake kama kisingizio cha kuchelewesha uchaguzi.

Kagame ambaye alikuwa kizungumza ndani ya Bunge Novemba 30, 2022, amesema Dunia nzima inailaumu Rwanda kwa migogoro hiyo, wakati Tshisekedi akijinufaisha kimamlaka kupitia mzozo huo wa kisiasa.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Picha ya The Independent Uganda.

Amesema, ukosefu wa usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaweza kupatiwa ufumbuzi ikiwa nchi moja inayojiandaa kwa uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka ujao (2023), haitautumia kama kisingizio cha hali ya dharura.

Mapigano hayo kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23, yamezidisha mvutano baina ya Serikali za DRC na Rwanda huku Kongo ikimtuhumu Kagame kuwaunga mkono waasi hao, tuhuma ambazo Rwanda imekuwa ikizikanusha.

Iptisam apata wastani 'A' mtihani darasa la saba
Wengi wanaishi na VVU bila kugundulika: WHO