Vinara wa Ligi Kuu ya England ‘Arsenal’ watarejea tena Uwanjani baadae juma ili, huku Fainali za Kombe Dunia zikiendelea kurindima nchini Qatar.
Arsenal itapasha misuli joto kabla ya kuendelea kwa Mshike Mshike wa Ligi Kuu ya England kwa kucheza Michuano maalum ‘Dubai Super Cup’ itakayoshirikisha timu nyingine tatu za Barani Ulaya.
Klabu ya Olimpic Lyon ya Ufaransa, AC Milan ya Italia, Arsenal na Liverpool zote za England zimealikwa kwenye Michuano hiyo ambayo rasmi itaanza siku ya Alhamis (Desemba 08) Dubai.
Hata hivyo katika Michuano hiyo timu za England (Arsenal na Liverpool) hazitakutana, na badala yake zitacheza dhidi ya timu nyingine shiriki kutoka Italia na Ufaransa.
Kwa sasa Ligi Kuu za Mataifa ya Ulaya zimesisimama kupisha Fainali za Kombe la Dunia, zitakazofikia tamati Desemba 18, huko nchini Qatar.