Mshambuliaji wa vinara wa Ligi Kuu ya England ‘Arsenal’ Gabriel Jesus atakuwa nje ya Dimba kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuumia kifundo cha mguu, na kuondolewa kwenye kikosi cha Brazil kinachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini Brazil ‘CBF’ imeeleza kuwa, Mshambuliaji huyo amerejea jijini London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo maalumu, ili kubaini ukubwa wa jeraha lake baada ya kuumia.
Madaktari wa Arsenal wamesema kuna uwezekano Jesus akafanyiwa opereshen ya kifundi cha mguu na atakaa nje ya Uwanja kwa muda wa miezi mitatu.
Kwa Mantiki hiyo Jesus atakosa michezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya West Ham baada ya Sikukuu ya Christmas, kabla ya kumenyana na Brighton na baadae dhidi ya Newcastle utakaochezwa Januari 3 mwaka 2023.