Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), imepokea mapendekezo toka Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuhusu viwango vya nauli za abiria kwa treni ya njia ya Reli ya Kisasa (SGR), ambapo LATRA pia inapanga kukusanya maoni ya wadau kabla ya kufikia uamuzi wa kuridhia.
Maoni hayo, yanatarajia kukusanywa Desemba 19, 2022, ambapo mapendekezo ya TRC yanaonesha nauli kutoka Dar es Salaam kwenda Soga daraja la kawaida kwa mtu mzima ni Shilingi 9,494, mtoto wa miaka kati ya 4-12 ni Shilingi 4,747 huku daraja la kati mtu mzima nauli ikiwa Shilingi 11,392 na mtoto Shilingi 5,696.
Jedwali la nauli hizo, pia linaonesha kutoka Dar es Salaam kwenda Ruvu nauli ni Shilingi 14,394, mtoto shilingi 7,197 kwa daraja la kawaida huku daraja la kati ikiwa ni Shilingi 17,272 na mtoto Shilingi 8,636 ambapo pia kutoka Dar es Salaam hadi Ngerengere nauli itakuwa ni Shilingi 19,494 na mtoto Shilingi 9,747 ambapo daraja la kati Shilingi 23,392 kwa mtu mzima na Shilingi 11,696 kwa mtoto.
Aidha, nauli kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro inapendekezwa kuwa Shilingi 24,794 na mtoto Shilingi 12,397 huku daraja la kati ikiwa ni Shilingi 29,752 kwa mtu mzima na kwa mtoto Shilingi 14,876 ambapo kwa Dar es Salaam hadi Mkata abiria daraja la kawaida atalipia Shilingi 30,194 na Shilingi 17,847 kwa mtoto.
Kutoka Dar es Salaam hadi Kilosa daraja la kawaida malipo ni Shilingi 35,694 kwa mtu mzima na mtoto ni Shilingi 17847 huku daraja la kati ikiwa ni Shilingi 42,832 mtu mzima na mtoto Shilingi 21,416 na Dar es Salaam kuelekea Kidete ikiwa Shilingi 41,394 na mtoto Shilingi 20,697 kwa daraja la kawaida.l
Kutoka eneo hilo pia kwa daraja la kati ni Shilingi 49,672 na mtoto Shilingi 24836 huku nauli kutoka Dar es Salaam hadi Gulwe ikiwa ni Shilingi 47,294 na Shilingi 23,647 na kwa daraja la kati ni Shilingi 56,752 na Shilingi 28,376 kwa mtoto ambapo kutoka Dar es Salaam hadi Igandu Sh53,294 na Sh26,647 kwa mtoto na daraja la kati ni Sh63,952 na kwa mtoto ni Sh31,976.
Jedwali hilo pia limeonesha nauli kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni Shilingi 59,494 kwa mtu mzima na Shilingi 29,747 kwa mtoto huku daraja la kati ikiwa ni Shilingi 71,392 kwa mtu mzina na mtoto ikiwa ni Shilingi 35,696 ambapo kwa umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Bahi nauli pendekezwa ikiwa Shilingi 65,894 kwa mtu mzina na mtoto Shilingi 32,947 ambapo kwa na kwa daraja la kati ni Shilingi 79,072 na mtoto Shilingi 39,536.