Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua kiwanda cha kuchakata maziwa cha MSS kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, ambacho kina uwezo wa kusindika wastani wa lita 10,000 za maziwa kwa saa.

Majaliwa amezindua kiwanda hicho hii leo Desemba 13, 2022 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ambapo pia ametoa rai kwa wafugaji wanaozunguka kiwanda hicho kuuza maziwa kwa mwekezaji huyo ili kujiongezea kipato na kumwezesha mwekezaji kuwa na uhakika wa kuzalisha bidhaa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha MSS Fresh Milk cha Nsimbo, Salum Maliki (kushoto)  baada ya kuzindua kiwanda hicho.  Kulia ni Mbunge wa jimbo la Nsimbo, Anna Lupembe.

Amesema, “Uwepo wa kiwanda hiki kunaisaidia kuendeleza mkakati wa lishe bora kwa kila Mtanzania, kwa sasa tunamshauri aendelee kupanua kiwanda hiki ili aongeze uzalishaji na wananchi wengi wazidi kupata ajira.”

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi inayojengwa katika eneo la Ilembo, Mpanda, ambapo alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imeendelea na mkakati wa kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kuhakikisha inajenga majengo ya ofisi ya mikoa na wilaya mpya Katavi ukiwemo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua kiwanda cha maziwa cha MSS Fresh Milk katika jimbo la Nsimbi Mkoani Katavi hii leo Desemba 13, 2022.

Majaliwa pia amesema, “Serikali itaendelea kuwatumikia na haitowaangusha sisi wasaidizi wa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia tutafanya kazi wakati wote, wakati wa jua kali na hata wakati wa mvua, tunataka kuhakikisha dhamira ya Rais wetu ya kuleta maendeleo inatimia.”

Awali, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema kuwa Rais Dkt. Samia ameridhia kutoa shilingi milioni 200 kupitia Bodi ya Maziwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ukusanyaji wa maziwa Mpanda, Katavi.

Serikali 'yavutwa shati' usambazaji wa pembejeo
Tanzania yaridhia uenyeji mkutano wa Kilimo