Zaidi ya watu 120 wamefariki jijini Kinshasa ambao ni mji mkuu wa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Maji jinsi yalivyoleta mafuriko kufuatia mvya kubwa jijini Kinshasa. Picha ya BBC.

Taarifa hiyo imetolewa Desemba 13, 2022 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinshasa, Sylvano Kasongo ambaye ameongeza kuwa wanahofiwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Wananchi wakitazama nyumba iliyobomolewa na mafuriko. Picha ya Stringer/ REUTERS

Amesema, Barabara kuu katika mji huo wenye wakazi zaidi ya milioni 15 zilifunikwa na maji huku picha zinazosambazwa mitandaoni zikionesha maporomoko ya udongo katika wilaya ya Mont-Ngafula na kusababisa mpasuko kwenye barabara muhimu inayounganisha mji huo na bandari ya Matadi.

Sehemu ya uharibifu uliofanywa na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, katika viungani vya jiji la Kinshasa, DRC Desemba 13,2022. Picha ya Stringer/ REUTERS.

Aidha, amesema Nyumba nyingi za mabanda zilizojengwa katika maeneo yenye hatari ya kukumbwa na mafuriko, zimeathirika pakubwa, huku vifo hivyo vikikumbusha tukio la mwaka 2019 ambapo watu 40 walifariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo.

Bunge kuamua hatma ya Ramaphosa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 14, 2022