Bunge nchini Afrika Kusini limejadili leo hoja ya ikiwa litaanzisha mchakato wa kuamua iwapo Rais Cyril Ramaphosa anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi ataondolewa madarakani.

Ramaphosa aliyekuwa akitizamwa kama mpambanaji dhidi ya rushwa baada ya mtangulizi wake ambaye utawala wake ulizongwa na kashfa za ufisadi Jacob Zuma, pia anakabiliwa na madai ya kujaribu kuficha fedha nyingi za wizi.

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Picha ya News24

Ripoti ya jopo huru la uchunguzi, imesema huenda Ramaphosa ana hatia ya ukiukwaji mkubwa wa sheria na utovu wa nidhamu, ikiwa ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa kwenye kikao cha bunge mjini Capetown.

Chama tawala cha ANC, kinamuunga mkono Ramaphosa na kimetaka jumla ya wabunge wake 230 kwenye bunge lenye wajumbe 400 kupinga kuondolewa kwake huku upinzani ukiungana kuhusu suala hilo na haijulikani ikiwa baadhi ya wabunge wa ANC, wataungana na upinzani.

Wahimizwa kuchangamkia fursa Chuo cha Madini
Watu 120 wafariki kwa mafuriko, maporomoko