Mkuu wa chuo cha Madini Nzega ambalo ni tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Nuru Msengese amewataka Wananchi wa Mkoa wa Tabora kuchangamkia fursa za masomo yanayotolewa na chuo hicho kwa mwaka wa masomo wa 2023.
Msengese ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza na kuongeza kuwa, tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho miaka mitatu iliyopita bado kasi ya udahili kwa wanafunzi wanaotoka Mkoa wa Tabora ni ndogo ukilinganishe na wale wanaotoka Mikoa mingine.
Kufuatia hali hiyo, Afisa tarafa ya Nyasa Wilaya ya Nzega Ricardo Komanya anasema kwa kushirikana na wadau mbalimbali wa Elimu wataongeza mbinu katika kukitangaza chuo hicho kwa wananchi ili kiweze kudahili wanafunzi wengi zaidi wakiwemo wa kutoka Mkoa wa Tabora.
Awali, Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Afisa Tawala Wilaya ya Nzega, Charles Makwaya aliwataka wanafunzi kufuata misingi na taratibu za chuo, ambazo zitawasaidia kufikia malengo yao na kuleta ufanisi katika soko la ushindani.