Kifo cha Mwandishi wa Habari wa TBC, Joachim Kapembe ambaye alifariki akiwa anashuka katika Mlimani wa Kilimanjaro hapo jana Desemba 13, 2022 kimesababishwa na ajali ya Baiskeli na si madhara ya kupanda Mlima Kilimanjaro kama inavyodaiwa.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ambaye amesema amesikitishwa na msiba huo na kwamba hadi wanafika kileleni kwa mafanikio hakukuwa na madhara ya kupanda mlima na wakati wakiteremka baaadhi ya watu waliamua kutumia Baiskeli akiwemo Marehemu Joachim.

Marehemu, Joachim Kapembe.

Amesema, “Nimesikitishwa sana na kifo cha Rafiki yangu Joachim Kapembe tuliyekuwa nae kwenye safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro, Kapembe amefariki kwa ajali ya baiskeli wakati akitoka katika kambi ya Kibo kuelekea kambi ya Horombo baada ya kupanda mlima hadi kufika kileleni kwa mafanikio na ni mmoja wa Watu ambao hawakupatwa na madhara ya kupanda mlima.”

Aidha, Msigwa ameongeza kuwa, “Baada ya kufanikiwa kufika kileleni Kilimanjaro na kushuka, Watu wote tulifika kambi ya Kibo ambako tulipaswa kuendelea kwenda kambi Horombo, wachache waliamua kutumia baiskeli badala ya kutembea kwa miguu akiwemo Joachim Kapembe bahati mbaya akiwa anateremka mteremko wa kutoka Kibo ndipo akapata ajali iliyosababisha apoteze maisha.”

Polisi wawatembelea wahanga ajali za Pikipiki
Ukandamizaji: Wanahabari 533 wafungwa jela